Sheria ya Tume ya Mipango Tanzania
Official PDF Document Download
Read full text
©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.447 SURA YA 127 SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SHERIA KUU] Mpangilio wa Vifungu Kifungu Jina sehemu ya kwanza MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Jina. 2. Matumizi. 3. Tafsiri. sehemu ya pili TUME YA MIPANGO 4. Kuanzishwa kwa Tume. 5. Muundo wa Tume. 6. Majukumu ya Tume. 7. Mamlaka ya Tume. 8. Akidi na taratibu za uendeshaji wa shughuli za Tume. 9. Posho na stahili. 10. Tume kudumisha ushirikiano. sehemu ya tatu MASHARTI YA UTAWALA 11. Uteuzi wa Katibu Mtendaji. 12. Naibu Makatibu Watendaji. 13. Uteuzi wa watumishi. 14. Kamati. 15. Mashauriano na Wizara yenye dhamana ya masuala ya fedha. sehemu ya nne MASHARTI YA FEDHA 16. Vyanzo vya fedha. 17. Makadirio ya mapato na matumizi na udhibiti wa fedha. 18. Matumizi ya fedha. 19. Bajeti ya nyongeza. 20. Hesabu na ukaguzi. 21. Taarifa ya mwaka. 17. Makadirio ya mapato na matumizi na udhibiti wa fedha. 18. Matumizi ya fedha. 19. Bajeti ya nyongeza. 20. Hesabu na ukaguzi. 21. Taarifa ya mwaka. ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.448SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] sehemu ya tano MASHARTI YA JUMLA 22. Mamlaka ya kutengeneza kanuni. 23. Kiapo rasmi. 24. Mamlaka ya kupata taarifa. 25. Wajibu wa kushirikiana. 26. Makosa na adhabu. sehemu ya sita MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI 27–34. Vimeondolewa. 24. Mamlaka ya kupata taarifa. 25. Wajibu wa kushirikiana. 26. Makosa na adhabu. sehemu ya sita MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI 27–34. Vimeondolewa. ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.449 SURA YA 127 SHERIA YA TUME YA MIPANGO Sheria ya kuanzisha Tume ya Mipango; kubainisha wajumbe wake na kuainisha majukumu na mamlaka yake; na kuainisha masuala mengine yanayohusiana na hayo. [15 Julai, 2023] [TS. Na. 476A la 2023] Sheria Na. 1 ya 2023 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Tume ya Mipango. 2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara. 3. 1 ya 2023 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Tume ya Mipango. 2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara. 3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Kamati ya Uteuzi” maana yake ni Kamati ya Uteuzi ya Tume iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 14(2); “Katibu Mtendaji” maana yake ni Mtendaji Mkuu wa Tume aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 11; “mpango mkakati” maana yake ni mpango ulioandaliwa na wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na taasisi nyingine za umma kwa mujibu wa miongozo iliyotolewa na Tume; “mjumbe” maana yake ni mjumbe wa Tume aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 5; “Mwenyekiti” maana yake ni Mwenyekiti wa Tume aliyetamkwa katika kifungu cha 5(1); “Rais” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Jina Matumizi Tafsiri na yake ni Mwenyekiti wa Tume aliyetamkwa katika kifungu cha 5(1); “Rais” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Jina Matumizi Tafsiri ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.450SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] “Tume” maana yake ni Tume ya Mipango iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 4; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya masuala ya mipango ya maendeleo ya taifa. SEHEMU YA PILI TUME YA MIPANGO 4.–(1) Inaanzishwa Tume itakayojulikana kama Tume ya Mipango. (2) Tume itakuwa idara inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais. 5.–(1) Tume itaundwa na Rais ambaye atakuwa Mwenyekiti na wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Rais kama ifuatavyo: (a) Waziri mwenye dhamana ya masuala ya mipango ya maendeleo ya taifa; (b) Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha; na (c) wajumbe wengine wanne ambao watakuwa wajumbe wa muda. (2) Tume inaweza kumualika mtu yeyote ambaye si mjumbe kushiriki katika vikao vya Tume na kutoa utaalamu au mchango mwingine wowote kama Tume itakavyoona inafaa. aweza kumualika mtu yeyote ambaye si mjumbe kushiriki katika vikao vya Tume na kutoa utaalamu au mchango mwingine wowote kama Tume itakavyoona inafaa. (3) Katika kuteua wajumbe wa Tume, uteuzi utazingatia watu wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha katika masuala ya uchumi na mipango ya maendeleo, ufuatiliaji na tathmini, utafiti na maendeleo au usimamizi wa masuala ya Serikali au ya umma na waliodhihirisha kuwa na uwezo wa kushughulikia masuala ya kitaifa na kimataifa. (4) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (5), mjumbe wa Tume, tofauti na Mwenyekiti, atakaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. Kuanzishwa kwa Tume Muundo wa Tume na Mwenyekiti, atakaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. Kuanzishwa kwa Tume Muundo wa Tume ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.451SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] (5) Bila kujali kifungu kidogo cha (4), nafasi ya mjumbe itakuwa wazi kabla ya kuisha kwa miaka mitano endapo- (a) kwa mjumbe ambaye ni Waziri, amekoma kuwa Waziri; (b) amejiuzulu kwenye nafasi yake kwa kutoa notisi ya maandishi kwa Rais; (c) amefariki; au (d) ameondolewa madarakani na Rais. 6.–(1) Tume itakuwa na wajibu wa kusimamia uchumi, mchakato wa upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya taifa kama ilivyoidhinishwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwa na ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa na maendeleo kama ilivyokusudiwa. aendeleo ya taifa kama ilivyoidhinishwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwa na ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa na maendeleo kama ilivyokusudiwa. (2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya kifungu kidogo cha (1), majukumu ya Tume yatakuwa ni- (a) kutathmini hali ya rasilimali za taifa na kuishauri Serikali kuhusu matumizi bora ya rasilimali hizo; (b) kuandaa dira ya maendeleo ya taifa, mpango wa maendeleo wa muda mrefu, mpango wa maendeleo wa muda wa kati na mpango wa maendeleo wa muda mfupi, na kusimamia utekelezaji wake; (c) kupendekeza maeneo ya miradi endelevu ya kielelezo na mikakati ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzingatia dira na mikakati ya maendeleo ya taifa; (d) kufanya tathmini na uchambuzi wa mara kwa mara wa viashiria muhimu vya uchumi ambavyo vinajumuisha urari wa malipo, mtiririko wa fedha na bei, deni la taifa na kuishauri Serikali ipasavyo; (e) kutathmini sera mbalimbali zilizopo kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wake kwa kuzingatia mipango ya maendeleo ya taifa na kupendekeza sera mpya pale inapoonekana inafaa kwa maslahi ya taifa; (f) kufuatilia utekelezaji wa maeneo muhimu ya vipaumbele vya taifa kwa sekta mbalimbali za uchumi na kuhakikisha kuwa hatua stahiki zinachukuliwa ili kutatua changamoto zozote za uendeshaji zitakazobainika katika sekta hizo; Majukumu ya Tume uchumi na kuhakikisha kuwa hatua stahiki zinachukuliwa ili kutatua changamoto zozote za uendeshaji zitakazobainika katika sekta hizo; Majukumu ya Tume ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.452SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] (g) kutoa mwongozo kuhusu ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa; (h) kuhakikisha mipango ya sekta inafungamanishwa na mipango ya taifa ili kuwa na matumizi yenye tija ya rasilimali za nchi; (i) kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango ya kitaifa na miradi ya kielelezo na kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi; (j) kuishauri Serikali kuhusu mabadiliko yoyote katika mpango wa maendeleo wa taifa ulioidhinishwa; (k) kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu masuala ya mipango ya maendeleo na usimamizi wa uchumi; (l) kushauri kuhusu mikakati ya kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu nchini; (m) kukuza mbinu za ubunifu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo; (n) kutambua na kufanya utafiti kuhusu suala lolote ambalo Tume inaona ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo ya taifa; (o) kusimamia na kutoa mwongozo katika uandaaji wa mipango mkakati iliyoandaliwa na wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na taasisi nyingine za umma; (p) kuratibu na kuendeleza kada za mipango, uchumi na takwimu na taaluma nyingine zinazofanana na hizo; (q) kuratibu makongamano ya wadau mbalimbali kwa ajili ya kujadili masuala ya mipango ya maendeleo; (r) kubainisha rasilimali za nchi kwa matumizi endelevu kwa maendeleo ya taifa; (s) kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo; na nchi kwa matumizi endelevu kwa maendeleo ya taifa; (s) kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo; na ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.453SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] (t) kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na mipango ya maendeleo kadri Rais atakavyoelekeza. (3) Bila kujali masharti ya Sheria nyingine yoyote, Tume, kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake chini ya Sheria hii, inaweza kuitisha mpango mkakati wowote ulioandaliwa na wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa au taasisi nyingine za umma kwa ajili ya mapitio na kutoa maelekezo ipasavyo; (4) Mpango wowote wa muda mfupi au wa muda mrefu ulioandaliwa kwa mujibu wa Sheria hii au sheria nyingine iliyotungwa na Bunge na kuidhinishwa na Bunge kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(c) ya Katiba hautabadilishwa au kuachwa kutekelezwa katika muda uliopangwa kutekelezwa bila idhini ya Bunge. 7. na Bunge kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(c) ya Katiba hautabadilishwa au kuachwa kutekelezwa katika muda uliopangwa kutekelezwa bila idhini ya Bunge. 7. Kwa kuzingatia masharti ya Katiba, Sheria za Tawala za Mikoa, Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na sheria nyingine yoyote inayohusiana na muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali, Tume itakuwa ndicho chombo cha juu cha ushauri katika masuala yote yanayohusiana na mipango ya maendeleo na usimamizi wa uchumi na kwa madhumuni hayo itakuwa na mamlaka ya- (a) kubaini na kuidhinisha maeneo ya vipaumbele muhimu vya maendeleo ya taifa na kutoa maelekezo ya kujumuishwa katika mipango ya maendeleo ya taifa na sekta na kwa utambuzi wa utekelezaji wake; (b) kutoa maelekezo na miongozo kwa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa au taasisi nyingine za umma, kuhusu masuala ya mipango ya uchumi na maendeleo kama ilivyoidhinishwa na Serikali; (c) kuitisha kutoka katika taasisi yoyote taarifa au takwimu yoyote zinazohusiana na masuala ya mipango ya maendeleo na usimamizi wa uchumi; na Mamlaka ya Tume Sura ya 2, 97, 287 na 288 yoyote taarifa au takwimu yoyote zinazohusiana na masuala ya mipango ya maendeleo na usimamizi wa uchumi; na Mamlaka ya Tume Sura ya 2, 97, 287 na 288 ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.454SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] (d) kutoa maelekezo na miongozo muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora na wenye ufanisi wa majukumu yake chini ya Sheria hii. 8.–(1) Katika kikao chochote cha Tume, akidi itakuwa nusu ya wajumbe waliopo kwa wakati huo. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1) na kanuni ambazo Mwenyekiti anaweza kutengeneza kwa ajili hiyo, Tume itakuwa na mamlaka ya kusimamia taratibu za uendeshaji wa shughuli zake. 9. Wajumbe wa Tume watalipwa posho na stahili nyingine kadri itakavyoamuliwa na mamlaka husika. 10. Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake, Tume itaanzisha na kusimamia mfumo wa ushirikiano na ushauri na taasisi na watu wengine, iwapo ni shirika au vinginevyo, na ikiwa ni ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano, watakaoweza kusaidia katika utekelezaji bora na wenye ufanisi wa majukumu yake chini ya Sheria hii. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA UTAWALA 11.–(1) Kutakuwa na Katibu Mtendaji wa Tume ambaye atateuliwa na Rais. fanisi wa majukumu yake chini ya Sheria hii. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA UTAWALA 11.–(1) Kutakuwa na Katibu Mtendaji wa Tume ambaye atateuliwa na Rais. (2) Katibu Mtendaji atakuwa Afisa Mtendaji Mkuu na Katibu wa Tume na atakuwa na wajibu wa kutekeleza majukumu ya Tume na kusimamia shughuli za kila siku za Tume. (3) Wakati wa kumteua Katibu Mtendaji, uteuzi utazingatia utaalamu wa uchumi, masuala ya mipango na fedha na uzoefu katika utawala na nafasi za juu za uongozi. Akidi na taratibu za uendeshaji wa shughuli za Tume Posho na stahili Tume kudumisha ushirikiano Uteuzi wa Katibu Mtendaji na nafasi za juu za uongozi. Akidi na taratibu za uendeshaji wa shughuli za Tume Posho na stahili Tume kudumisha ushirikiano Uteuzi wa Katibu Mtendaji ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.455SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] 12.–(1) Kutakuwa na Naibu Makatibu Watendaji wa Tume watakaoteuliwa na Rais kwa idadi itakayohitajika katika wakati husika. (2) Naibu Makatibu Watendaji watamsaidia Katibu Mtendaji katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya Katibu Mtendaji kama watakavyopangiwa na Tume. 13.–(1) Watumishi wataajiriwa na Tume kwa misingi ya ushindani na kwa idadi kadri inavyohitajika kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Tume. (2) Maafisa wa Tume, isipokuwa wajumbe, watakuwa ni watumishi wa umma. 14.–(1) Tume inaweza kuunda kamati kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake na inaweza kukasimu majukumu yake yoyote kwa kamati yoyote iliyoundwa. (2) Bila kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (1) na masharti ya kifungu cha 11 na 12 na bila kujali sheria nyingine yoyote, kwa madhumuni ya kuwezesha mchakato wa uteuzi wa wajumbe wa Tume, Katibu Mtendaji, Naibu Makatibu Watendaji na watumishi wengine wa Tume, kutakuwa na Kamati ya Uteuzi ambayo uteuzi na majukumu yake yataainishwa katika kanuni. endaji, Naibu Makatibu Watendaji na watumishi wengine wa Tume, kutakuwa na Kamati ya Uteuzi ambayo uteuzi na majukumu yake yataainishwa katika kanuni. (3) Kamati iliyoanzishwa chini ya kifungu hiki, endapo itaona inafaa na kwa kuzingatia idhini ya Tume, inaweza- (a) kumshirikisha mtu yeyote kuwa mjumbe wa Kamati kwa kipindi kitakachoainishwa; na (b) kumualika mtu yeyote kuhudhuria kikao chochote cha Kamati. 15. Tume itaweka utaratibu wa mashauriano na Wizara yenye dhamana ya masuala ya fedha ili kuhakikisha utekelezaji bora wa miradi ya maendeleo kama ilivyoainishwa katika mipango ya maendeleo ya taifa. Naibu Makatibu Watendaji Uteuzi wa watumishi Kamati Mashauriano na Wizara yenye dhamana ya masuala ya fedha shwa katika mipango ya maendeleo ya taifa. Naibu Makatibu Watendaji Uteuzi wa watumishi Kamati Mashauriano na Wizara yenye dhamana ya masuala ya fedha ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.456SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] SEHEMU YA NNE MASHARTI YA FEDHA 16. Fedha za Tume zitajumuisha- (a) kiasi cha fedha kitakachotengwa na Bunge; (b) ruzuku zitakazotolewa na Serikali; na (c) mapato mengine yoyote. 17.–(1) Katika kipindi kisichopungua miezi mitatu kabla ya mwisho wa kila mwaka wa fedha, Katibu Mtendaji ataandaa na kuwasilisha bajeti kwa Tume kwa ajili ya kuidhinishwa itakayojumuisha makadirio ya mapato na matumizi kwa ajili ya mwaka wa fedha unaofuata. (2) Tume inaweza kumtaka Katibu Mtendaji kufanya marekebisho katika bajeti ikiwa kwa maoni yake bajeti haiakisi makadirio sahihi na ya kuridhisha ya mapato na matumizi. 18. Matumizi hayatafanyika kutoka kwenye fedha za Tume isipokuwa kama matumizi hayo ni sehemu ya matumizi yaliyoidhinishwa na Tume chini ya kifungu cha 17(1) kwa mwaka wa fedha husika. 19.–(1) Wakati wowote kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha husika, Katibu Mtendaji anaweza kuandaa na kuwasilisha kwa Tume makadirio yoyote ya nyongeza kwa ajili ya kuidhinishwa kwa mwaka husika. waka wa fedha husika, Katibu Mtendaji anaweza kuandaa na kuwasilisha kwa Tume makadirio yoyote ya nyongeza kwa ajili ya kuidhinishwa kwa mwaka husika. (2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), endapo imetokea dharura kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume, Katibu Mtendaji anaweza kufanya matumizi ambayo hayajaidhinishwa na Tume kwa idhini ya Mwenyekiti na katika mazingira hayo, Katibu Mtendaji atatakiwa ndani ya miezi mitatu baada ya kufanya matumizi hayo, kuomba idhini ya Tume. 20.–(1) Katibu Mtendaji atatunza vitabu vya hesabu na kuhifadhi kumbukumbu sahihi za uendeshaji wa Tume kwa mujibu wa viwango vya uhasibu. Vyanzo vya fedha Makadirio ya mapato na matumizi na udhibiti wa fedha Matumizi ya fedha Bajeti ya nyongeza Hesabu na ukaguzi u wa viwango vya uhasibu. Vyanzo vya fedha Makadirio ya mapato na matumizi na udhibiti wa fedha Matumizi ya fedha Bajeti ya nyongeza Hesabu na ukaguzi ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.457SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] (2) Ndani ya miezi sita baada ya mwisho wa kila mwaka wa fedha, Katibu Mtendaji ataandaa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume katika mwaka huo wa fedha na nakala moja ya taarifa hiyo pamoja na nakala ya hesabu zilizokaguliwa zitawasilishwa kwa Tume. (3) Hesabu za Tume zitakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali au mtu mwingine aliyeteuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa madhumuni hayo. 21. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali au mtu mwingine aliyeteuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa madhumuni hayo. 21. Ndani ya miezi miwili baada ya kupokea taarifa ya hesabu zilizokaguliwa na taarifa za mkaguzi wa hesabu kuhusu hesabu hizo, Tume itamuelekeza Waziri kuwasilisha Bungeni ndani ya miezi miwili au katika kikao cha Bunge kinachofuata nakala ya taarifa ya mwaka kuhusu mwaka huo wa fedha ikijumuisha- (a) nakala ya hesabu zilizokaguliwa za Tume pamoja na taarifa ya mkaguzi kuhusu hesabu hizo; (b) taarifa ya utekelezaji wa malengo ya msingi na taarifa nyingine yoyote inayohusiana nayo; (c) taarifa ya shughuli za Tume katika mwaka wa fedha husika; na (d) taarifa nyingine yoyote kadri Tume inavyoweza kuelekeza. SEHEMU YA TANO MASHARTI YA JUMLA 22.–(1) Waziri anaweza kutengeneza kanuni kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya Sheria hii. (2) Bila kuathiri ujumla wa masharti ya kifungu kidogo cha (1), Waziri anaweza kutengeneza kanuni zinazoainisha- (a) muundo, uteuzi na masuala mengine kuhusu Kamati ya Uteuzi; (b) ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya taifa; Taarifa ya mwaka Mamlaka ya kutengeneza kanuni e kuhusu Kamati ya Uteuzi; (b) ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya taifa; Taarifa ya mwaka Mamlaka ya kutengeneza kanuni ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.458SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] (c) miongozo ya uandaaji wa mipango mbalimbali inayotakiwa kuandaliwa chini ya Sheria hii; (d) suala lingine lolote ambalo ataona linafaa kwa utekelezaji bora wa Sheria hii. 23.–(1) Kabla ya kuanza kutekeleza majukumu, kila mjumbe wa Tume, Katibu Mtendaji na Naibu Katibu Mtendaji, atatakiwa kuapa kwa mujibu wa sheria husika. (2) Masharti ya kifungu kidogo cha (1) hayatamhusu Mwenyekiti. 24. Tume, kwa maandishi, inaweza kumtaka mtu yeyote au kikundi cha watu ambao wana taarifa yoyote muhimu ambayo inayohusiana na majukumu yake- (a) kuwasilisha taarifa au kutoa nyaraka husika kadri Tume itakavyoainisha; au (b) kuhudhuria mbele ya Tume kwa ajili ya ushauri au ufafanuzi kuhusu taarifa au nyaraka hizo. 25.–(1) Kila mtu atakuwa na wajibu wa kushirikiana na Tume kadri itakavyohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mamlaka, kazi na majukumu yake. ka hizo. 25.–(1) Kila mtu atakuwa na wajibu wa kushirikiana na Tume kadri itakavyohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mamlaka, kazi na majukumu yake. (2) Katika utayarishaji wa mpango mkakati, wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na taasisi nyingine za umma zitazingatia miongozo iliyotolewa na Tume. 26. Mtu yeyote ambaye- (a) anatoa taarifa au takwimu zozote huku akijua kuwa ni ya uongo au kutoa taarifa au nyaraka ambazo kimsingi si sahihi kwa nia ya kuipotosha Tume; (b) anaizuia Tume kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi chini ya Sheria hii; au (c) bila kibali cha maandishi kutoka Tume, anachapisha au kufichua maudhui ya nyaraka yoyote, mawasiliano au taarifa za aina yoyote ambazo amezifahamu wakati wa utekelezaji wa majukumu yake chini ya Sheria hii kwa Kiapo rasmi Mamlaka ya kupata taarifa Wajibu wa kushirikiana Makosa na adhabu ezifahamu wakati wa utekelezaji wa majukumu yake chini ya Sheria hii kwa Kiapo rasmi Mamlaka ya kupata taarifa Wajibu wa kushirikiana Makosa na adhabu ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.459SHERIA YA TUME YA MIPANGO [SURA YA 127 TOLEO LA 2023] mtu yeyote asiyeidhinishwa au vinginevyo tofauti na utekelezaji wa majukumu yake, anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi milioni kumi au kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka mitano. SEHEMU YA SITA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI [Vifungu vya 27–34 Vimeondolewa]Vimeondolewa ©2025 Government of Tanzania. All rights reserved. No part of this book may be reproduced or distributed without permission of OAG.
Have questions about this law?
Ask Ubutabera AI for instant, cited answers — free with an account. Save laws and download official PDFs too.
Create a free account